Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Pandit Vijay Kumar Sharma, mhadhiri na mwanaharakati wa kidini wa Kihindu, ambaye pia ni miongoni mwa wanaharakati wanaouunga mkono Muqawama wa Palestina, aliyesafiri nchini Iran kushiriki katika hafla ya kihistoria ya kumuaga na kumsindikiza Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alisema katika hotuba yake huku akisisitiza juu ya uhuru wa mataifa na kupinga ubeberu wa madola makubwa ya kimataifa:
“Mimi kama raia wa India na mfuasi wa dini ya Kihindu, ninaamini kwamba mataifa yanapaswa kushirikiana kwa msingi wa kuheshimiana, uadilifu na heshima ya utu wa mwanadamu. Madola makubwa hayapaswi kuamua hatima ya nchi nyingine, wala hakuna nchi yenye haki ya kulazimisha mapenzi yake kwa wengine kwa kutumia nguvu na mashinikizo.”
Akizungumzia shakhsia ya Ayatullah Khamenei (ra) alisema: “Yeye alikuwa mfano wa uongozi wenye maisha ya unyenyekevu na wa kiroho, aliyechipuka kutoka miongoni mwa watu wa kawaida, na daima alisisitiza kuwatetea wanyonge na kulinda uhuru wa nchi. Maisha yake ya kawaida na ukaribu wake na tabaka za watu wasiojiweza ni miongoni mwa sifa ambazo watu wengi duniani huziheshimu.”
Kiongozi huyo wa kidini wa Kihindu aliendelea kwa kuzungumzia suala la Palestina na maendeleo ya Mashariki ya Kati, akisema: “Leo watu duniani wana maswali mazito kuhusu mateso ya wananchi wa Palestina. Historia ya Karbala na msimamo wa Imam Hussein (as) ni alama ya kusimama dhidi ya dhulma na kutokukubali maridhiano mbele ya dhuluma kwa watu wengi, bila kujali dini au madhehebu yao.”
Pia alikosoa vita na uingiliaji wa kigeni nchini Iran, akiongeza: “Wananchi wa kawaida, watoto na wazee wanahitaji amani, si vita wala uharibifu. Uzoefu wa miaka iliyopita umeonesha kwamba migogoro mingi ya kisiasa na tamaa zisizo na mipaka zimechangia kuharibiwa kwa nchi na kuwafanya watu wengi kuwa wakimbizi. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kufuatilia mazungumzo na amani badala ya kuongeza mivutano.”
Kumar Sharma alisema katika sehemu nyingine ya hotuba yake: “Hata kama madola yote makubwa yataungana upande mmoja, bado haifai kunyamazia vitendo vyao visivyo vya kisheria na visivyo vya haki. Misingi ya maadili na ubinadamu haipaswi kutolewa kafara kwa ajili ya maslahi ya kisiasa. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa; ninazungumza kwa mtazamo wa kibinadamu na wa kiroho.”
Aliongeza: “Dunia ya leo inawahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote viongozi kama Ayatullah Khamenei (ra) ambao kwa maisha yao ya unyenyekevu, maadili mema na kuwajali wananchi, wamekuwa mfano thabiti wa amani na uadilifu.”
Maoni yako